Mtaani kuna siri ambayo wachuuzi wametuficha kwa muda na hakuna mpishi wa nyumbani anaeza kuielewa: kwa nini smokie na yai boilo ukichanganya na kachumbari ya barabarani huwa tamu, lakini ukijaribu kuipika nyumbani inaladha tofauti?
Ukweli ni kwamba ata uende madukani, ununue smokies zilezile, vitunguu fresh, nyanya safi, upige ustarabu wa Michelin chef — bado utaishia kulia. Ni kama hawa wachuuzi wa barabarani wana uchawi wa ladha.
Siri iko kwa vibe. Mtaa ni spice yenyewe: vumbi ya lami, moshi wa matatu, makelele za watu kwa foleni, na yule mchuuzi wa kibanda akipiga nduru, “pili pili ama unataka plain?” Hiyo vurugu ndio inatoa ladha ya ukweli. Huwezi kufungia kikapuni.
Nyumbani? Usafi. Kimya. Umestaarabika kama paka wa dukani. Hakuna chembe ya vumbi kutia ladha, hakuna mtu anakusumbua shingoni akiuliza “Boss, yote shingapi?” Ile presha na haraka ya mtaa inachanganya kiojo.
Na hiyo sufuria ya mchuuzi, jameni! Imepitia miaka ya mafuta yaliyochemka, vitunguu vimeungua, machozi ya customer waliopewa balance mbaya. Sufuria hiyo iko na historia. Yako ya non-stick? Inaoga na sunlight kila siku hadi imepoteza roho yote.
Halafu peer pressure. Ukiwaona watu tano wenye njaa wanamaliza smokie na mayai hapo barabarani, ubongo wako unachemka unasema, “Boss, life is for the living!”
Kwa hivyo tusijidanganye. Ladha si chumvi peke yake, si kachumbari, wala pilipili. Ni fujo mtaani, ni jamii, ni utamaduni. Hapo ndipo smokie za barabarani zinaeza kushinda.
Smokie na mayai za mtaa si chakula tu. Ni uhuru wetu. Ni identity yetu wakenya.